Skip to Content

KUSAIDIKA KIFEDHA KWA WANAFUNZI

Maelekezo ya Kusaidika kifedha kutoka kwetu kwa Wanafunzi Wanufaika wa bumu

Wanafunzi wanufaika wanaotaka kusaidika kifedha wanapaswa kufuata hatua zifuatazo:

Hatua ya Kwanza: Kutafuta Mdhamini

1. Tafuta Mdhamini: Mwanafunzi anapaswa kutafuta mdhamini ambaye atamthibitisha na kusaidia katika mchakato mzima. Mdhamini anapaswa kuwa mtu mwenye uwezo wa kifedha na ambaye anaweza kutoa dhamana. Mfano, mdhamini anaweza kuwa mwanafunzi mwenye bumu.

Hatua ya Pili: Kuandaa Nyaraka

2. Andaa Picha za Passport Size: Mwanafunzi atahitaji kuandaa picha moja ya passport size. Pia, mdhamini atapaswa kuandaa picha moja ya passport size. Picha hizi zitahitajika katika fomu ya maombi.

Hatua ya Tatu: Kujaza Fomu ya Maombi

3. Jaza Fomu ya Maombi: Mwanafunzi atahitaji kujaza fomu ya maombi. Fomu hii italetwa mahali mwanafunzi anapoishi. Mwanafunzi anapaswa kujaza fomu hiyo kwa uangalifu, akihakikisha kuwa taarifa zote ni sahihi. Ili kupata fomu hii, utalipia ada ya fomu. Ikiwa mwanafunzi hatokuwa na ada hiyo, pesa hiyo inaweza kukatwa moja kwa moja kutoka kwenye fedha atakayopewa mwanafunzi kwa idhini yake.

Hatua ya Nne: Kuwasilisha Maombi

4. Wasilisha Fomu ya Maombi: Baada ya kujaza fomu, mwanafunzi atapaswa kuwasilisha fomu hiyo pamoja na picha za passport size za mwanafunzi na mdhamini. Pia, mwanafunzi anapaswa kuwasilisha nyaraka nyingine zinazohitajika kama vile kopi ya kitambulisho cha chuo.

Hatua ya Tano: Kupata fedha

5. Subiri Uthibitisho: Baada ya kuwasilisha maombi, mwanafunzi atahitaji kusubiri uthibitisho kutoka kwa taasisi. Uthibitisho huu utachukua takribani dk 30.

6. Kupata fedha: Mara baada ya maombi kupitishwa, mwanafunzi atapokea fedha yake. Hii itajumuisha taarifa kuhusu kiasi cha fedha na masharti ya urejeshaji.

Hatua ya Sita: Urejeshaji wa Mkopo

7. Rejesha fedha: Mwanafunzi atawajibika kurejesha fedha aliopewa. Urejeshaji utaanza baada ya mwanafunzi kupata bumu kama mnufaika. Ni muhimu kufuata masharti ya urejeshaji ili kuepuka usumbufu. Marejesho hayo yatakuwa ni ya awamu moja tu.

Sign in to leave a comment